SERIKALI YAITAKA KAMPUNI YA GAS ENTEC TANZANIA KUZINGATIA MKATABA.

SERIKALI imeuelekeza uongozi wa  Kampuni ya  Gas Entec Tanzania ambayo inajenga meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi  Tu kuzingatia makubaliano  yote   yaliyomo kwenye mkataba wa ujenzi wa meli hiyo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa  Kassim Majaliwa leo Mei 14, 2022  katika kikao kati yake na Balozi wa Korea ya Kusini nchini, Kim Sun